HATUA YA 214: Mtu Huyu Unamwachaje?

Imekuwa ni tabia ya wengi kukutana na watu mnazungumza mengi sana kuhusu Maisha na wakati mwingine kufahamiana kwenye mambo mbalimbali ya Maisha. Sasa ni vyema uwe unajiuliza ukiwa peke yako je unapenda kumueleza nini mtu yule ambaye umekutana nae kwa mara ya kwanza? Ungependa mtu huyu aondoke na picha gani kuhusu wewe? Hapa ni kutokana […]

HATUA YA 209: Hii Ndio Siri ya Kutoingia Kwenye Madeni.

Inawezekana Umekuwa Mtumwa wa madeni na hayaishi kila siku unajikuta unatengeneza madeni mapya. Suluhisho sio kuwa na pesa nyingi bali ni kuwa na nidhamu. Kwasababu hata ukiwa na pesa nyingi kama una tabia inayokuingiza kwenye madeni utajikuta unaendelea nayo kila wakati. Usinunue kitu chochote ambacho Hukupanga. Kitu chochote unachokutana nacho njiani kiwe kizuri kiasi gani, […]

HATUA YA 208: Unatumiaje Kidogo Ulichonacho?

Kabla Hujawaza kupata laki tano ya kuanzia biashara anza kuonyesha uwezo wako wa kutumia elfu hamsini. Kama ukishindwa kujua utaitumiaje elfu hamsini hata laki tano utashindwa kuitumia vizuri. Watu wengi tumekuwa tunalalamikia tatizo la mtaji  lakini tatizo sio mtaji tatizo lipo kwenye akili yako. Ili uweze kupata kile kikubwa unachokitaka jifunze kutumia kidogo kilichopo karibu […]

HATUA YA 207: Maneno Unayotakiwa KUJISEMESHA MWENYEWE UNAPOAMKA ASUBUHI

Kujisemesha mwenyewe ni njia nzuri sana ambayo unaweza kuitumia kutengeneza siku ambayo ni bora sana. Vile vile kwa kujisemesha mwenyewe kutakuasaidia USIISHIE NJIANI kwenye lile jambo uliloamua kulifanyia kazi. KUJISEMESHA MWENYEWE ni tiba ya akili na moyo wako hasa pale unapokuwa umeanza kupitia magumu katika kuitimiza ndoto yako. Unapopitia hali mbaya labda ni hasara kwenye […]

HATUA YA 203: MILIKI MAISHA YAKO

Kama kuna mtu  kila anachosema au anachotaka unaitika ndio, bila kuangalia kipo kwenye utaratibu au hakipo,  kitaathiri ratiba zako au maisha yako au lah. Huyo mtu ameyadhibiti maisha yako. Kama unasema ndio ili kumridhisha mtu na moyo unaumia kwasababu tu ya kitu unachokitegemea kwake huna umiliki na maisha yako. Usikubali kuwa na maisha ambayo yanategemea […]

HATUA YA 202: Ondoka Nyumbani.

Sehemu uliyoizoea ndio inafanya uwe na hali uliyonayo sasa hivi. Kama hapo ulipo unapata kila unachokitaka jiulize je utaendelea kupata unachokitaka kwa muda gani? Kama ukiona hakuna  muda mrefu hatua unayopaswa kuchukua ni kuondoka. Nyumbani kwako kunaweza kuwa ni kazini kwako pamoja na mshahara unaopokea. Inawezekana unadanganyika na mshahara unaopokea ukafikiri maisha yatakuwa hivyo siku […]

HATUA YA 201: Ukitaka Kutumia Zaidi..

Kanuni ya Umaskini ni kutumia Zaidi ya unachozalisha. Kama unataka kubakia kuwa maskini endelea kuwa na matumizi makubwa kupita uwezo wako wa kuzalisha. Kama wewe ni mkulima ukizoea kula Zaidi ya unachozalisha mwisho wa siku utakula na mbegu inayokuzalishia. Kama wewe ni mfanyabiashara ukizoea kutumia Zaidi ya unachopata utaanza kula mtaji. Kanuni ya mafanikio inasema […]

HATUA YA 200: Pima Kazi Yako Hivi.

Leo ni siku ya 200 mfululizo tangu nimeanza kuandika. Unaweza kufikiri ni kitu rahisi lakini sio kitu rahisi maana ili uandike lazima ujilazimishe kufikiri sana. Sasa kama mtu ni mvivu kufikiri hawezi kuandika kila siku. Lakini ni kwambie siri iliyopo nyuma ya hizi hatua 200? Wakati naanza nilifika hatua kama ya 50 hivi wakajitokeza watu […]

HATUA YA 197: Tengeneza Mazingira.

Kuku anapotaka kutaga kwa mara yake ya kwanza lazima atafute sehemu nzuri na aitengeneze ili aweze kutaga vizuri. Kwa bahati mbaya sana kuku hana akili hivyo anaweza kujitafutia sehemu yeyote tu hata nje ya banda lake. Ila kwa mfugaji anaejua kitu anafanya lazima awaandalie kuku wake mazingira ya kutaga pale wanapohitaji kutaga. Kipindi Fulani kuku […]

HATUA YA 196: Kuna Mahali Ulisababisha.

Mambo mabaya yote yanayotokea kwenye Maisha yako sio kwa bahati mbaya kuna mahali uliyasababisha yakatokea. Badala ya wewe kuchukua muda mwingi kulaumu na kulalamika jiangalie kwa upande wako unahusikaje kusababisha. Tuchukue mfano rahisi watu wawili wanagombana hadi kutaka kupigana, ukikaa na mmoja wapo ukamuuliza ilikuaje ataanza kumtupia lawama mwenzake. Lakini ukweli hadi wakafikia kugombana yeye […]