Pata GREENHOUSE Kwa bei ya OFa

Kwa mwezi huu wa March na April tunatoa OFA ya Punguzo la ujenzi wa Greenhouse. Ni punguzo la gharama ya ya ujenzi wa Greenhouse. Punguzo la bei litakua kuanzia 10% hadi 30% kutegemeana na ukubwa wa greenhouse. Vilevile ofa hii itaambatana na Ongezeko la vifaa au huduma, mfano tank la maji, kuunganisha na soko nk. […]

SURA YA 440: Usichanganye na Maji.

Miaka kama 10 iliyopita Kulikuwa na bibi mmoja kijijini kwetu alikuwa anauza maziwa fresh. Maziwa yake yalikuwa ni matamu sana na pia masafi hivyo kusababisha watu wengi kuyapenda na kuyasemea vizuri. Kadiri watu walivyoyasemea vizuri ilifika wale waliokuwa wanauza maziwa kama yeye ikabidi wafunge kwa kukosa wateja. Watu Karibu mtaa mzima ulihamia kwake. Bibi yule […]

KONA YA BIASHARA: Faida za Kuwa na Maono Kwenye Biashara Yako

Pasipo maono kwenye biashara yeyote watu wengi huishia njiani. Kama hakuna unapotaka kufika utakuwa unaridhika na kile unachokipata kila siku. Kama huna maono huwezi kuwa na mipango mipya wala mabadiliko labda tu hali iwe mbaya. Biashara nyingi zilizokosa maono huendeshwa kiholela, wamiliki wa biashara na hata wafanyakazi hawajui ni wapi wanataka kwenda. Wengi wanaishia kuangalia […]

#KONA YA BIASHARA: Unachoweza Kufanya Ni Kipi?         

Unaweza kuwa na sababu za kila aina zinazoelezea kwanini hadi sasa huna unachokifanya au hujamiliki biashara yako. Swali langu kwako litakuwa ni unachoweza kufanya ni kipi? Tukiacha hizo sababu unazotoa je hakuna hata kitu kimoja kidogo unaweza kufanya? Hakuna kweli? Hakuna unachojua Zaidi ya wengine hapo mtaani kwenu kweli? Hakuna biashara inayoendeshwa hovyo hovyo hapo […]

KONA YA BIASHARA: Yajue Mapungufu Yako.

Ni vyema kwa kila mmoja akaweza kutambua ni wapi ana mapungufu na kuyafanyia kazi kabla hayajaleta madhara kwenye kazi. Kila binadamu ana mapungufu yake ndio maana haupo mwenyewe huku duniani. Kuna sehemu unateleza na yupo mtu ataweza kuwa msaada wako. Unapoyajua mapungufu yako unajipa nafasi ya ushindi mzuri kwenye biashara yako. Ukae ukijua kwamba mapungufu […]

KONA YA BIASHARA: Ukipoteza Hii Inakuja Nyingine.

Kuna nyakati kwenye Maisha unaweza kujiona umepoteza vitu vikubwa sana na ukaanza kuona kama Maisha hayana maana tena. Unachopaswa kutambua ni kwamba kila kinapoondoka kitu basi kuna kitu kingine kipya kinatokea. Mti unapokauka unakuwa umetoa nafasi kwa miti mingine mingi midogo kukua vizuri. Chochote kinachoondoka kwenye Maisha yako kinatengeneza nafasi iliyowazi kwa ajili ya vitu […]

KONA YA BIASHARA: Lijue Dhumuni La Biashara Yako.

Kama jinsi kulivyo na magari ya abiria, mizigo na binasfi vile vile biashara zipo kwa madhumuni ya aina mbalimbali. Ni vyema wewe kama mfanyabiashara ukalijua dhumuni la biashara yako kwenye jamii uliyopo. Jiulize unawasaidia nini watu kwa biashara yako? Unajua mtu hawezi kwenda kununua gari la abiria wakati mahitaji yake ni gari la kutembelea. Hivyo […]

KONA YA BIASHARA: Hiki Ndio Sababu ya wewe Kuanguka Kibiashara

Kinachoshangaza sana kwa biashara nyingi za kwetu ni kwamba wamiliki au walioajiriwa kwenye biashara ndio wanaongoza kwa kudharau, kuongea vibaya na wateja wao. Mteja anapoamua kuja kwenye biashara yako sio kwamba ana shida sana, wewe ndio una shida na hela ndio maana ukafungua hiyo biashara, ungekuwa huna shida na pesa ungekaa nazo nyumbani ukatumia. Mteja […]

KONA YA BIASHARA: JINSI YA KUPATA MTAJI NA KUANZA BIASHARA YAKO

Kuna mambo machache unatakiwa ujiulize Je eti ni kweli mwaka ujao utakuwa mpya kwako au ni zile kelele tu na hamasa? Una kitu gani unakitegemea kukipata cha tofauti ndani ya mwaka ujao? Umeajiandaa vipi kukipata? Upo tayari kuwa mpya ili upate hayo mambo mapya ya mwaka ujao? Tuachane na hayo twende kwenye mada yetu ya […]

KONA YA BIASHARA: TABIA ZA KUKUWEZESHA KUFIKIA MAFANIKIO NA BIASHARA YAKO

Mwaka ndio huoo unakwisha umefikia wapi na malengo yako? Yaani ndio hivyo mwaka unaishaga ni sekunde moja inacheza na kutengeneza dakika na dakika nayo inakwenda hadi masaa 24. Kunakuwa asubuhi, mchana, jioni na hatimaye usiku siku inapita. Hivyo ukidhani kuna kitu cha tofauti kwenye mwaka mpya utakuwa unakosea. Utofauti wa mwaka unaweza kuwa ni majira […]