KONA YA BIASHARA: Makosa 3 Unayofanya na Yataua Biashara yako.

Leo kwenye kona ya biashara tunaangalia makossa matatu ambayo unafanya na yataua biashara yako siku si nyingi. Kama kawaida ni mambo madogo sana ambayo yanaweza kusababisha ukapoteza kila ulichonacho hasa kama yatakuja taratibu na kuleta madhara bila ya wewe kujua na ukaja kutambua madhara yakiwa makubwa kabisa. Kuna baadhi ya makossa unayafanya yanakuwa kama kansa […]

KONA YA BIASHARA: Hakuna Uhakika 100%.

Katika mambo tunayofanya kila siku kwenye Maisha yetu pamoja na kuwa na imani kubwa, hamasa na matarajio makubwa hakuna mwenye uhakika asilimia mia moja kwamba mambo yatakuwa sawa. Ndio mambo yanaweza kuwa vile ulivyopanga lakini sio asilimia mia. Unachopaswa kujua ni kwamba kwa kila maamuzi unayofanya ni hatari unachukua hivyo tarajia chochote kile kinaweza kutokea. […]

KONA YA BIASHARA: Ongezeka Wewe Kwanza.

Kwenye biashara nyingi unaweza kukutana na watu wanalalamika biashara zao hazikui, hakuna kinachoongezeka hali ni ile kwa muda mrefu. Ukija kuchunguza Zaidi unakutana na shida nyingine kwamba mmiliki wa biashara mwenyewe hajakua. Unachotakiwa kufahamu ni kwamba biashara haiwezi kukua inakuzidi wewe. Kile kiwango cha ukuaji wa biashara yako ni kiwango chako cha ukuaji. Ule uwezo […]

KONA YA BIASHARA: Neno  Samahani Linavyombakisha Mteja.

Kinachofanya ubaki kwenye soko sio jina lako kubwa ulilonalo, sio bidhaa yako nzuri peke yake. Kuna vitu vya ziada lazima ufanye ili uendelee kubaki. Bahati mbaya sana usipofanya yupo mwenzako ana biashara kama yako atafanya na atakuchukulia wateja wako. Bahati mbaya sana kama unafikiri huna mshindani bado hata kesho unaweza kumuona mtu mwingine amekuja hapo […]

KONA YA BIASHARA: Kama Una Tabia Hizi Usishangae Kwanini Hukui kibiashara.

Zipo Sababu nyingi za kushindwa kwa biashara mbalimbali lakini hizi ni mojawapo ya vyanzo vinavyofanya watu washindwe. Kama unataka kuwa na mafanikio tengeneza tabia njema ambazo zinawavutia wengi kuwa karibu na wewe.  Kukasirika Hovyo Hasa Mteja Anapokuja na Malalamiko. Kama unashindwa kuvumilia malalamiko ya wateja wako una hatari kubwa ya kuwapoteza wote. Jaribu kuwa msikivu […]

KONA YA BIASHARA: Biashara ni Zaidi ya Kuuza.

Unapowaza kuuza pekee kwenye biashara unakosa vitu vingine vya muhimu sana. Biashara ni kutatua matatizo ya wengine. Biashara ni kuyafanya maisha ya wengine kuwa bora Zaidi ya yalivyo kuwa. Biashara ni kugusa maisha ya wengine. Usikae kwenye biashara kwa lengo la kuuza tu. Embu ona unatatua jamii yako inayokuzunguka. Ona ukiyafanya maisha ya wengi kuwa […]

KONA YA BIASHARA: Ukuaji ni Hatua Kwa Hatua.

Shida kubwa haipo kwenye biashara mara nyingi shida kubwa ipo ndani yako. Unajua kwanini nasema hivyo? Kama biashara unayoifanya wewe kuna mwingine anaifanya vizuri kuliko wewe na ana mafanikio shida haipo kwenye biashara shida ipo kwako. Shida ipo kwako kwasababu hutaki kufuata hatua unataka kuruka ufike kule unakotaka. Unataka kukimbia wakati bado hujakomaa kwenye kutembea. […]

NAMNA YA KUWEZA KUFIKIA MAFANIKIO NA BIASHARA YAKO

Habari za leo Rafiki? Ni siku nyingine tena ya Baraka sana kwangu. Natumaini na kwako ni ya baraka Pia. Tunapopata nafasi ya kuwa na nguvu ya kuendelea kufanya yale tunayafanyayo ni vyema sana kushukuru.   Mwaka ndio huoo unaanza kwenda wewe unaelekea wapi? Leo ni tarehe 9 siku tisa zimeshapita wewe umeshaanza kuacha alama gani […]

Wateja Hawa wanakupotezea Muda

Habari za leo Ndugu natumaini unaendelea vyema na majukumu yako. Ninachofahamu ni kwambakila mmoja kuna kitu anauza hata kama umeajiriwa unauza ujuzi wako kwa mwajiri wako. Lakini leo nakwenda kuzungumzia juu ya wateja na changamoto walizonazo.   Mteja anaekwambia kwamba atachukua au ataanza bila kuweka Commitment yeyote ya tarehe au siku ambayo atachukua bidhaa au […]

Jinsi ya kupata wazo la biashara:

Habari za leo ni matumaini yangu kua unaendelea vyema kabisa. Leo tunakwenda kutazama njia tano za kupata wazo la biashara popote pale ulipo. Karibu ujifunze nami. Zipo njia tano ambazo unaweza kuzitumia kubuni wazo bora la biashara katika jamii uliyopo nayo ni: •       1. Kwa kuangalia baadae(future): Kwa kuangalia jamii unayoishi unaweza kugundua baadae mabadiliko yatakuaje […]