411; Wewe ni Hodari Kwenye Nini?

Kila mtu kuna sehemu ambayo ni Hodari sana kuliko sehemu nyingine. Na hili ndio mojawapo ya mambo yanayotutofautisha wanadamu, unaweza kuwaleta watu kumi wanaofanya kitu kimoja ambacho kinafanana kabisa lakini unakuta kila mmoja ana sehemu ambayo yeye ni Hodari kuliko wengine. Si vyema kabisa kumdharau mwenzako kwasababu ya kile ambacho unadhani unakijua kuliko yeye kumbuka […]

410; Unastahili, Usiangalie Nje Yako.

Kuna nyakati unaweza kukutana na fursa mbele yako kabisa halafu ukapishana nayo kama vile hukuiona kwasababu unajiona hustahili. Kuna mambo makubwa yanaweza kujisogeza karibu yako kwasababu ni Mungu anayaleta na anajua wewe unastahili hayo ila kwasababu unajiona wewe ni mdogo sana, wewe ni dhaifu sana hivyo hata uwezo wa kuona fursa ile unakuwa haupo. Inawezekana […]

409; Imani Yako Itakuponya au Itakuua.

Katika Biblia vitabu vya Injili tunamwona Bwana Yesu akitenda miujiza kwa kuwaponya vipofu, viwete,na wenye madhaifu ya aina mbalimbali. Siku moja mwanamke alietokwa na damu kwamiaka 12 alipoamua kwenda kulishika vazi la Yesu akiamini kwamba ataponaalipona kweli. Yesu akamwambia Imani yako imekuponya. Ni kweli Imani yake NdioIlimponya. Tukiangalia nyuma kabla hajaamua kwenda kumshika Yesu alikuwa […]

408; Utaweza Kuvumilia?

Inawezekana unayatazama Maisha ya watu waliofanikiwa na kujikuta unatamani sana kuishi kama wao na kujiona wewe unaishi Maisha ambayo ni duni sana. Ukweli ni kwamba kuna ambao wanatamani wangekuwa na Maisha ya kawaida kama yako kwasababu ya changamoto kubwa wanazokutana nazo sehemu ambazo wapo. Kama unafikiri utaweza kuvumilia kuandikwa vibaya kwenye magazeti kwa habari ambayo […]

407; Naomba Nikukumbushe tena Hili.

Yapo mambo ambayo ni msingi wa Maisha bora ya kila mwanadamu, kama ukiweza kuyafanyia kazi vizuri utaishi kwa furaha na amani hapa duniani siku zote. Ni kweli yapo mambo mengi mabaya yanatokea bila sisi kujua na tunakuwa hatuna uwezo wa kuzuia lakini ukiweza kufuata hii misingi utaweza kuwa na Maisha bora. Mambo haya ndio yanayofanya […]

406; Ni rahisi Sana Kuanza, Tabu Ipo Hapa.

Watu wamekuwa wanasema mwanzo ni mgumu ni kweli kuna baadhi ya mambo mwanzo ni mgumu. Ila bado kuna mambo ambayo ni rahisi sana kuanza ila kumaliza vile ambavyo unataka ndio imekuwa changamoto ya wengi. Unaweza kuwa na mawazo makubwa na mipango mikubwa wakati unaanza mwaka lakini unapofika mwisho unajikuta hujafanya hata robo ya kile ambacho […]

405; Sio Lazima Ufanane Nao

Furaha itakuja pale ambapo utaanza kuishi Maisha ambayo moyo wako unataka na sio vile ambavyo watu wanataka uishi. Furaha ya kweli ipo ndani yako na utaweza kuipata kwa kuishi kile ambacho Mungu ameweka ndani yako. Hakuna haja ya kuishi Maisha vile ambavyo jamii inakulazimisha wewe uishi, vile jamii ambavyo imetengeneza na kutoa maana ya Maisha. […]

404; Ni Wachache Sana Wanaweza Kujibu Swali Hili.

Ukimuuliza mtu akutajie mambo 3 ya muhimu sana kwenye Maisha yake ni wachache wataweza kukujibu kwa usahihi nikiwa na maana kwamba walikuwa wanayajua kabla hujawauliza. Ni rahisi mtu kujibu kwa kutamka kile ambacho kitamjia kichwani kwa wakati huo lakini ukweli ni kwamba utakuta hafanyi chochote katika hayo aliyosema ni ya muhimu kwenye Maisha yake. Embu […]

403; Maneno Yao Sio Uhalisia Wako.

Wanaweza Kusema yule jamaa alifeli shule hajaweza kufika hata chuo hawezi chochote. Wanaweza kusema yule dada kila mahusiano yamemshinda hawezi kutulia na mwanaume. Wanaweza kusema pia pombe zitakuja kukuua siku moja. Wanaweza kusema wewe ni mtu wa maneno maneno sana na huwa unaongea vitu visivyoeleweka. Hayo yote na mengine ambayo wanaweza kusema juu yako ni […]

402; Mtu Huyu Anakudanganya.

Ulishawahi kutaka kukutana na mtu akakujibu kwamba hana muda? Umewahi kujiuliza ni kwanini anasema hana muda? Je kuna ukweli wowote pale anapokwambia hana muda? Wanadamu wote tumepewa masaa 24 kila siku na hii ni mojawapo ya vitu ambavyo kila mmoja anacho kwa usawa kabisa. Kinachotutofautisha ni yale ambayo tunatumia kwenye muda wetu kila siku. Kuna […]