494; Endapo Maisha Yote Uliyoishi Mpaka Sasa Yangekuwa ni Ndoto.

Habari Rafiki, leo naomba ujiulize swali hili la msingi sana. Iwapo umeamka asubuhi halafu ukajitazama ukakuta umerudi nyuma miaka 10 au ishirini iliyopita. Yaani kumbe yote yaliyotokea kwenye Maisha yako miaka kumi iliyopita ilikuwa ni ndoto tu ulikuwa unaota usiku wa jana. Swali la msingi la kujiuliza je hiyo ndoto itakuwa inatamanisha kuwa kweli? Je […]

493; USIWATHIBITISHIE. (DON’T PROVE THEM WRONG)

Kwa muda mrefu nimekuwa nikiona watu wanafanya vitu mbalimbali kama ujasirimali, biashara fulani, kazi Fulani, ili tu kuwathibitishia watu fulani waliokuwa wanawaona wao hawafai. Mfano mtu aliambiwa wewe hujawahi kuweza kitu hutaweza biashara. Anaingia kwenye biashara kwa hasira ili tu amthibitishie yule mtu kwamba anaweza. Unaweza kuambiwa wewe huwezi kupata kazi Fulani kwasababu huna elimu […]

492; UTABAKI KAMA ULIVYO USIPOBADILI IMANI.

Tumekuwa tukiishi kutokana na picha ambazo tumejengewa na wale watu tulio waamini sana. Watu hawa wanaweza kuwa ni wazazi wetu, ndugu zetu, viongozi wet una hata waalimu wetu. Kila mmoja amekuwa akituaminisha kwa jinsi alivyoelewa na kuamini. Yako mengi yamekuwa ni makossa na yameendelea kufuatishwa hivyo hivyo bila kujali au yeyote kujiuliza hivi hii ni […]

491; Waache Waondoke.

Kuna aina ya watu wanaweza kuja kwenye Maisha yako na kusababisha upoteze kabisa muelekeo wa Maisha. Kile ambacho umekuwa unakipigania na kukisimamia kikaanza kushuka na kupotea. Ni vyema kuwatambua watu wa namna hii mapema kabla hawajachukua nafasi kubwa na kukufanya uwe mtumwa kwao na kusahau kile ambacho ulizaliwa kuja kufanya hapa duniani. Wapo waliongia kwenye […]

490; KABLA HUJAMFANYIA MTU UBAYA JARIBU KUONA KWA JICHO HILI.

“Nakumbuka siku moja nikiwa hapa Arusha kabla sijaoa nilipanda daladala kuelekea Tengeru kwenye shughuli zangu za kila siku. Ninaishi Arusha Sanawari hivyo magari mengi ya Tengeru huja yakiwa matupu ili yapakie abiria kwenye kituo cha Sanawari. Siku hiyo kulikuwa na kimvua kidogo ambacho kiliwafanya watu wakimbilie kwenye magari haraka yanapofika tu kituoni. Na mimi nilikuwa […]

489; Hizi Ndio Fikra Zinazokufanya Usiendelee Kwenye Maisha.

Ndani ya jiji lenye watu wengi kuliko miji mingine ndani ya Tanzania jiji la Dar es Salaam, kumekuwa na changamoto kubwa sana ya Usafiri. Hivyo basi serikali pamoja na watu binafsi wamekuwa wakiwaza kila siku ni njia gani inaweza kuwa suluhisho la tatizo hili. Katika kufikiri huko kukatokea watu wawili ambao walikerwa sana tatizo hili […]

488; Usiongeze Matumizi, Ongeza Hiki.

Badala ya kubadilisha aina ya maisha unayoishi baada ya kuongezeka kwa kipato Wekeza zaidi kwanza. Badala ya kukununua vitu ambavyo vitakuongezea matumizi ya pesa zaidi nunua vitu ambavyo vitakurahisishia kupata pesa zaidi. Badala ya kuongeza wanawake wengi Wekeza Kwenye baadae ya watoto wako. Badala ya kutaka kila mtu ajue umepata pesa weka nguvu kubwa zaidi […]

487; KUNA WATU UMEWAZIDI VITU VINGI, LAKINI WANAFANIKIWA, ZIJUE SABABU ZINAZOKUKWAMISHA.

Umeshawahi kusikia mtu anasema, “Mbona kama wamempendelea yule! sionagi cha maana anachokifanya wala simuelewagi!!” Mwingine anadiriki kusema, “Atakuwa ametoa rushwa kuipata ile nafasi”, “Atakuwa anajuana na mtu kule ndio maana amependelewa” Je na wewe unafikra za aina hii? Ukiona wenzako wanafanya vizuri unafikiri wamependelewa au wana bahati Fulani? Haujawahi kuamini kwamba watu hawa wamefanikiwa kwa […]

486; Makosa Matatu Wanayofanya Wengi Baada ya Kuumizwa Kwenye Mahusiano.

Kwanza nataka ujijengee mtazamo huu kwenye akili yako, tatizo lolote linapotokea kwenye Maisha yako usiwe mwepesi sana kuona wengine ndio wanahusika, anza kuona wewe umehusikaje, imekuaje ukawa katikati ya tatizo hilo. Kuwepo katikati ya tatizo ina maanisha kuna mahali wewe ulikosea hadi ukafika hapo. Ukisalitiwa inamaanisha kuna mahali ulikosea ukajikuta uko kwenye kusalitiwa, ndio unaweza […]

485; Unafikiri Kwanini Utahukumiwa Wakati Hukuja Duniani Kwa Maamuzi Yako?

Leo nakumbuka siku yangu ya kuzaliwa, nimetimiza miaka kadhaa hapa duniani. Katika kutafakari mambo mbalimbali na kujiuliza maswali nilijikuta katika mawazo haya, “Mimi sijawahi kumuomba Mungu aniumbe binadamu, sasa inakuaje nikikosea ameahidi adhabu mbalimbali?” kwanini niadhibiwe kwa Maisha ambayo hata sijayachagua kuishi? Ukweli ukitafakari hayo maneno yako kama yana ukweli Fulani ndani yake. Lakini hupaswi […]