SURA YA 427; Njia Rahisi ya Kuwavuta Watu Sahihi Kwako.

Tupo kwenye dunia ambayo ni ngumu sana kumjua mtu kwasababu wengi wamevaa mavazi yanayofunika uhalisia wao. Wamevaa tabia za kuigiza ambazo sio za kweli na wala hawana kabisa. Wamevaa Maisha ambayo ni uongo na ndani yake wanateseka huku wakifurahia kuona watu wanawasifia. Sasa ili uweze kuwavuta watu sahihi na kuwaacha hawa waliojivalisha mavazi ya uongo […]

418; Fanya Kitu Hiki Muhimu Siku Chache Zilizobakia Mwaka Huu.

Pamoja na kwamba inawezekana unaona kama mwaka huu mambo hayajaenda sawa kabisa na malengo mengi hayajatimia bado una nafasi ya kumaliza mwaka vizuri sana. Kuna mambo machache tu ukiamua kuyafanya kwa siku hizi zilizobaki baki unaweza kupata furaha kubwa sana ndani ya moyo na ukajisikia utoshelevu. Watazame wale ambao unawapenda inawezekana ni mwenzi wako, Watoto, […]

Pata Zawadi ya Kitabu.

Habari Rafiki yangu, ni matumaini yangu kwamba unaendelea vyema na Maisha. Leo nataka nikupe zawadi nzuri sana ya kitabu. Kitabu ambacho utakisoma msimu huu wa siku kuu na kikusaidie uongeze Maarifa ya kuukabili mwaka 2019. Ili upate zawadi hii mwishoni mwa Makala hii kuna sehemuimeandikwa JIUNGE NASI. Hapo utatakiwa uweke email yako na kisha ubonyeze […]

414; Hujachagua Kuzaliwa, Hujui Utakufa Lini, Unaweza Kimoja Tu.

Maisha ni ya ajabu sana, unazaliwa bila idhini yako mwenyewe, pengine hata wazazi wako hawakutarajia wala kupanga wewe uzaliwe. Na hata kama wakipanga hawawezi kujua kabisa ni mtu wa aina gani anazaliwa, vipimo vinaweza kujua jinsia lakini haviwezi kujua ile jinsia imebeba mtu wa namna gani. Kingine cha ajabu sana sasa ni kuwa hujui utakufa […]

413; Huwezi Kutatua Usichokifahamu.

Mimi ni fundi wa kompyuta, inapotokea kompyuta ninayotumia imezima ghafla siwezi kukimbilia kwenda kubadili ule mfumo unaoendesha kompyuta nzima (windows). Hiyo inaweza kuwa ni suluhisho lakini kabla sijafanya hivyo lazima kwanza nianze kujua tatizo ni nini na limesababishwa na kitu gani. Kujua tatizo ndio kutanipa mwangaza wa suluhisho la aina gani linatakiwa. Katika Maisha yako […]

Ni wewe Mwenyewe Umechagua 18/11/2018.

“Mwaka 2016 tulikuwa kwenye msiba wa jirani yetu ambaye alifiwa na mama yake. Siku hiyo watu walikuwa wanalia sana na kusikitika kwa kifo kile kilichotokea. Kitu kimoja ambacho kilimshangaza kila mtu ni kwamba mtoto wa kiume wa marehemu alikuwa hana machozi na wala hana huzuni sana kama ambavyo wengi walidhani itakuwa hivyo. Watu wakajikuta wanajiuliza […]

400: Hakuna AnaeKulazimisha.

Ulipokuwa mtoto kuna nyakati ulikuwa ukichelewa kuamka unakuja kuamshwa na viboko au wakati mwingine unamwagiwa maji. Kuna wakati pia ulikuwa unalazimishwa kusoma kwa bidii na unaambiwa uweke maji kwenye beseni ili usisinzie. Naomba ujiulize hivi sasa ni nani tena anaekulazamisha tena ufanye kazi kwa bidii ili uwe na pesa? Ni nani tena anaekuja kukuamsha mapema […]

398: Kuwa Mkweli Kwako Kwanza.

Unaweza kuwadanganya wengine lakini huwezi kujidanganya wewe mwenyewe. Ndani ya nafsi yako unajua ukweli ni upi. Ndani ya nafsi yako unajua kama Maisha unaigiza au ni kweli kile ambacho unakionesha. Mojawapo ya vitu vinavyowatesa wengi ni kujaribu kujidanganya wenyewe, unakuta unajua kabisa Matendo yako hayaashirii kabisa kile ambacho unataka lakini unajitia moyo wa uongo kwamba […]

397: Jinsi ya Kuondoa Imani Potofu Ambazo Ulijengewa Ukiwa Mtoto.

Mtu anatengenezwa katika umri wa kuzaliwa mpaka anapokuwa na miaka 7. Tabia Nyingi na Imani ambazo unazo sasa zilijengwa ulipokuwa mtoto. Na mara Nyingi Imani hizi zilijengwa ulipokuwa unaona kile ambacho watu wa karibu na wewe wanafanya. Mtoto anapozaliwa ubongo wake wa kumbukumbu unakuwa mtupu kabisa. Hivyo kila ambacho anaona kinafanyika kinaingizwa kwenye ubongo wa […]

Malengo Yako Yamefikia Wapi? Tumebakiwa na Robo Mwaka Sasa.

Habari Rafiki yangu. Utakuwa umeshtuka sana kusoma kichwa cha Makala hii, ukweli ni kwamba mwaka 2018 ndio umeisha hivyo. Tunasema imeabaki miezi miwili kwasababu mwezi wa 12 hatujauweka kwenye ratiba watu wengi ndio huenda likizo za kazi, wengi ndio mwezi wa kusherehekea. Itaendelea kubaki miezi mitatu kwa wale ambao wana biashara zao binafsi na lazima […]