Hali Itakapokuwa Mbaya..

“Kinachokupa Matumaini na Kiburi ni hali nzuri uliyonayo sasa hivi” Bahati mbaya sana unajisahau kwamba unachokitegemea ipo siku kinaweza kuwa na ukomo. Usisubiri hali iwe mbaya ndipo uanze kutafuta njia nyingine ya kipato, Usisubiri Mambo Yaharibike ndipo ukumbuke kuchukua hatua, jiandae mapema kwasababu hakuna anaepanga mabaya lakini siku zote tunayaona yakitukuta. Hali itakapokuwa mbaya ndipo […]

Haijalishi Una kipaji Kizuri Kiasi gani Unahitaji Kitu Hiki.

Watu wenye mafanikio makubwa duniani, ambao tunawaona ni matajiri waliweza kugundua siri hii kubwa na ya muhimu kwa kila mtu mwenye wazo au kipaji kizuri ndani yake. Kitakachokufanya ufanikiwe sio uzuri wa kipaji chako, sio sauti yako nzuri ya kuimba, sio watu wengi wanaokujua. Lazima ugundue siri hii ya muhimu, ambayo ndio iliwatoa wengi sana […]

Umetengeneza au Umeruhusu wewe mwenyewe.

Kabla hujaanza kusoma Makala hii naomba ujiulize swali hili, yale mambo ulikuwa unasemaga nitafanya kesho umeshayafanyaga hata japo nusu yake? Najua jibu la wengi ni hapana. Hata Makala hii kuna wengi walisema watasoma baadae na hawatasoma tena. Rafiki yangu mafanikio huwezi kuyapata bila ya Nidhamu. Nidhamu ni kufanya jambo ambalo unatakiwa kulifanya kwa wakati unaotakiwa […]

HATUA YA 291: Fikra Chanya, Matendo Chanya.

Your Positive Action Combined with Positive Thinking Results in Success. – Shiv Khera Matendo yako chanya yakijumuishwa na mawazo yako chanya yanaleta matokeo kwenye mafanikio. Kama unataka kufanikiwa lazima uzitangatie mambo haya mawili, mawazo chanya na matendo chanya. Kama utakuwa na mawazo chanya peke yake bila ya matendo huwezi kupata matokeo mazuri ya mafanikio. Vilevile […]

Mbinu Hii Itakuwezesha Upate Chochote Unachokitaka.

Kuna rafiki yangu mmoja nilikutana nae akaniambie “nyie mnaandika mbinu za mafanikio lakini hakunaga mbinu mpya zote ni zile zile tu.”  Kitu cha kushangaza ni kwamba mtu huyu bado na yeye hana chochote ambacho anakipigania yaani yupo yupo tu. Ukienda mbele Zaidi ukamuuliza kama mbinu ni zilezile wewe umeshatumia ipi ikakusaidia kati ya hizo unazozijua? Anakujibu […]

Usisubirie Tukio Tengeneza Tukio.

Hutaweza kufikia kamwe ndoto zako kama wewe ni mtu ambaye unasubiria tukio Fulani litokee ndipo uchukue hatua. Kama Maisha yako yatakuwa yanaendeshwa na matukio bila ya mipango huwezi kwenda mbele. Badala ya kusubiria tukio ndio likusukume kuchukua hatua anza kuchukua hatua sasa hivi. Hilo unalodhani litatokea kinaweza lisitokee kweli. Wanadamu wanaweza kutabiri mwaka huu mvua […]

Maisha yako ni Tabia Zako.

Maisha yako ni vile vitu ambavyo unavifanya kila siku ana kwa kuvifanya kila siku vinakwenda kuwa tabia yako. Muunganiko wa tabia zako unatengeneza kitu kinaitwa mfumo wa maisha. Huu mfumo wa maisha ni muunganiko wa tabia ndogo ndogo ambazo unazifanya kila siku. Kama tabia zako ni mbaya basi mfumo wako wa maisha utakuwa mbaya. Kama […]

Ukiteseka Duniani Utakwenda Kufurahi Mbinguni?

Inawezekana umekuwa na fikra hizi potofu kwamba ukiishi duniani maisha yenye dhiki, machozi na mateso kila siku basi utakwenda kuishi Maisha ya raha kule mbinguni. Ukweli ni kwamba kama umeshindwa kuishi kwa furaha hapa duniani unaweza kujuta Zaidi huko unapokwenda. Sio vibaya kutazamia mazuri kule tunapokwenda lakini ni muhimu kutambua thamani ya Maisha yetu hapa […]

Usiwe na Tabia za Maji.

Maji hayana umbo wala rangi, ukiyaweka kwenye chombo chochote kile yatachukua rangi ya chombo na umbo la chombo. Ukiyamwaga chini yatachukua vilevile rangi ya pale uliyoyamwaga. Maji siku zote hayana utaratibu yanafuata mkondo uliopo mbele na kuanza kutiririka. Pia yasipowekewa utaratibu mzuri huleta uharibifu mkubwa. Maji hayawezi kupanda mlima siku zote yanakimbilia mabondeni, ukitaka kuyapandisha […]

Unajisogeza Kwenye Shimo…

Mafanikio hayamtaki mtu mvivu, mtu mzembe, anaeahirisha mambo, anaetazama Zaidi kule alipotoka kuliko anapokwenda. Mafanikio yanamtaka mtu ambaye ameamua kutoka moyoni mwake kuwa anayataka mafanikio. Usikubali kabisa kuingia kwenye mtego wa kuchanganya mambo, kama umeamua kuwa muumini wa mafanikio amua kweli na uzifuate kanuni na misingi. Ukiwa mtu wa kuchanganya mambo, leo unataka hiki kesho […]