JINSI YA KUISHINDA TABIA YA KUISHIA NJIANI KWENYE MAISHA YAKO.

Tabia ya kufanya jambo kidogo kisha ukaona hakuna matokeo na ukakata tamaa na kwenda kukimbilia kufanya jambo jingine inaweza kuwa sababu ya wewe kutokutimiza chochote kwenye Maisha yako. Kama huna uwezo wa kufanya jambo moja hadi ukahakikisha limekuletea matokeo anza mapema kuitengeneza. Zipo sababu nyingi unaweza kuwa nazo za kwanini umeishia njiani lakini ukweli sababu […]

Usiliweke Moyoni Jambo Hili..

Unawajibika kwa kila hali inayoendelea kwenye Maisha yako. Lolote linalotokea kwenye Maisha yako wewe unahusika kwa asilimia mia moja kabla hujatupa lawama kwa mwingine yeyote. Unaweza kuamua uwe na furaha au uwe na huzuni. Unaweza kuamua kuwapenda wengine, kutenda wema kwa wengine au kufanya kinyume chake. Kuna jambo moja pekee ambalo unaweza kufanya ili uweze […]

Jinsi Ambavyo Kuchelewa Kufanya Maamuzi Kunavyoweza Kukuongezea Ugumu Wa Kufanya Maamuzi.

Katika mambo ambayo yanaweza kuwa sababu ya kila mtu mwenye mafanikio kufika pale alipo ni tabia hii ya kufanya maamuzi kwa wakati. Kama umeambiwa tafiti zinasema mwaka huu mvua hazitanyesha nyingi hivyo watu wapande mazao yanayovumilia mvua. Halafu wewe ukakazana kubaki unasubiria mvua ndugu yangu utakosa vyote au ukija kufanya maamuzi utakosa kiwango ulichopaswa kuvuna […]

UnaPata Muda wa Kukaa na Kuongea na Wewe?

“Vile nilivyojieleza kwako kuhusu mimi mara nyingi inaweza kuwa ni vile nilivyotaka wewe unifahamu mimi lakini inaweza kuwa mimi halisi sio huyo niliekuelezea.” Jacob Mushi Tumekuwa tunapata muda wa kukaa na watu, muda wa kazi, muda wa kuperuzi na kujua yanayoendelea duniani lakini mara chache sana tumekuwa tunapata muda wa kukaa na sisi. Kiwango unachojifahamu […]

KWANINI BINADAMU HATUWEZI KUFANANA KIFIKRA?

Maisha yako ni shule ambayo wengine watakuja kujifunza siku sio nyingi. Ulivyoishi maisha yako ndio itaamua uwe shule ya watu wengi kiasi gani. Kila ambacho unakifanya kila siku jiulize unakuja kuacha darasa la namna gani kwa wengine? Ukitenda mabaya utakuwa mfano mbaya, ukiweza kufikia ushindi wako utakuwa mfano wa kuigwa.  Moja ya jukumu unalopaswa kujipa […]

Jifunze Kwa Mtoto

Kuna nyakati kwenye maisha tunapitia hali ambazo zinatulazimisha kufanya mambo tusiyohitaji ila ni kwasababu tunaisikiliza mili yetu. Sio kila hali ambayo unaisikia kwenye mwili wako inahitaji kufanyiwa kazi. Ukiwa na mtoto mdogo utaweza kuniambia kwamba sio kila anacholilia mtoto unampatia. Mfano anatakiwa kulala na yeye anataka kwenda kucheza huwezi tu kumruhusu kwasababu ametaka. Anatakiwa kula chakula akalilia […]

Msamiati Huu Unatakiwa Uufute Kichwani Ili uweze Kutoka.

Kuna wimbo ambao umekuwa unaimbwa na watu wengi sana hasa linapokuja swali ni kwanini hujaweza kuanza biashara au kile ambacho unataka kufanya. Wimbo huu umekuwa ndio kikwazo kikubwa cha wengi kiasi kwamba wanabaki pale pale walipo siku zote. Sina Mtaji ni neon ambalo kama kweli una nia na mafanikio basi hutakiwi kulitamka mdomoni mwako tena […]

Ni Nini CHanzo cha Ndoto Zako?

Heri ya Mwaka Mpya Rafiki, Wakati tumeanza leo mwaka mpya napenda ujiulize swali moja la muhimu sana. Je ni nini chanzo cha ndoto zako? Unafahamu ndoto zako zimetoka wapi? Kuna wengine ndoto zao zimetokana na kukataliwa, kuachwa, kuonekana hawawezi na kadhalika. Maisha yao yote wanapambana ili siku moja waje wawaonyeshe wale waliosema hawawezi kwamba wanaweza. […]

WEWE NI NYOTA.

“Wewe ni nyota popote pale ulipo hakikisha unang’ara” Jacob Mushi 2018. Mwaka huu haijalishi upo sehemu gani unafanya kazi ya aina gani bado unahitajika kuonyesha kile kilichopo ndani yako. Haijalishi unaishi Maisha ya hali gani bado unatakiwa kuendelea kuonyesha kwamba wewe ni wa thamani. Dhahabu ikitupwa kwenye takataka bado inaendelea kubakia ni dhahabu. Haibadilishwi na […]

Unapanda Mbegu Gani?

Maneno yetu tunayosema mbele za watu ni mbegu, ipo siku yataleta matokeo. Vile unavyozungumza mbele za watu ndivyo watu wanatafsiri kuwa uko hivyo. Kama maneno ni mbegu basi unavyoyapanda mioyoni mwa watu tegemea matokeo yake siku moja. Hakuna mbegu ambayo haioti kama imetupwa kwenye udongo ikapata na maji. Chunga sana unavyoropoka mbele za watu maneno […]