536: Huwezi Kuwaridhisha.

Watu wanaweza kukuchukia pasipo na sababu yoyote ya msingi. Inawezekana hata hujawahi kuwasemesha lakini wakakuchukia. Inawezekana hujawawahi kuwatendea jambo lolote lile baya au la kuudhi lakini wakakuchukia tu. Unapaswa tu kutambua kwamba hata ufanye mambo mema kiasi gani hapa duniani huwezi kupendwa na kila mtu. Huwezi kumridhisha kila mtu. Unaweza kuzungumza sentensi moja ikamsaidia mtu […]

528; HEKIMA: Hakuwa Wako.

Kama alikuumiza kisha akaondoka hakuwa wako. Au tunaweza kusema muda wake wa kuendelea kuwepo kwako ulifika na njia ya kuondoka kwa ilikuwa lazima wewe uumie kwasababu haukujiandaa kuondoka kwake. Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi. Lakini walitoka ili wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu. 1 YOHANA. […]

527; HEKIMA: Kinyozi Anapokosea Kukunyoa.

Kinyozi anapokosea kukunyoa bila kujali amekosea kiasi gani siku zote baada ya muda Fulani nywele huota tena na utaweza kunyoa vile unavyotaka. Unapopoteza fedha haijalishi ni nyingi kiasi gani kama ni wewe mwenyewe ulizitafuta basi utaweza kuzipata tena. Unapoachwa na mpenzi ambaye ulimpenda sana bila kujali alikuwa mzuri kiasi gani, bado ipo siku utakuja kukutana […]

526; HEKIMA: Sumu Niliyowekewa Kwenye Chakula.

“Ilikuwa ni siku za mwisho wa mwaka ambapo tulikuwa na utaratibu wa kwenda kuwasalimia ndugu na jamaa ambao hatujawaona miaka mingi. Katika kuwatembelea ndugu jamaa na marafiki wengi siku moja nikapitia kwa ndugu mmoja ambaye hatukuonana muda mrefu sana. Huyu ndugu baada ya kunipokea alinisisitiza sana nile chakula. Nilimkatalia kwasababu nimepita nyumba nyingi na nimeshakula. […]

525; HEKIMA: Ni Wewe.

Ni wewe utawajibika pale unapoingia kwenye matatizo bila kujali ni nani aliyeyasababisha. Ni wewe utatakiwa kuchukua hatua pale mambo yanapokuwa magumu kwasababu ya uzembe unaoufanya sasa. Ni wewe utakalipa gharama za ulaji mbovu unaokula sasa pale utakapoanza kusumbuliwa na magonjwa. Ni wewe utakaelipa gharama ya ujinga unaoundekeza sasa hivi, unaambiwa ujifunze hutaki, Unaambiwa uweke akiba […]

524; HEKIMA: Panda Mti

Katika kutafakari sana siku ya leo juu ya Maisha yetu hapa duniani, nimekutana na jambo hili la ajabu sana. Nasikia kabisa Mungu anasema nikwambie, nizungumze na wewe ambaye umekata tamaa katika sehemu mbalimbali za Maisha yako. Unajua unaweza kufanya vitu vya aina mbalimbali vyote vikaharibika bila kukuletea mafanikio yoyote. Njia rahisi unaweza kuchagua ni kukata […]

523; HEKIMA: Uzima Ni Fursa

Kuna mtu yupo hospitali anamlilia Mungu ampe uzima ulionao, halafu wewe ni mzima na unakata tamaa. Jacob Mushi Unapotaka kukata tamaa kumbuka kwamba kuna watu ambao wanalilia nguvu ulizonazo sasa hivi. Kuna mtu anaipigania pumzi ya mwisho ili angalau aendelee kuwa hai. Nataka ujue kwamba uzima ulionao ni fursa kubwa sana kwasababu ni nafasi ya […]

522; HEKIMA: Kabla Hujakata Tamaa

Jaribu Tena, ndio nasema jaribu tena bila kujalisha umeshajaribu mara ngapi. Jaribu tena ukiwa na uhakika kwamba kuna jipya ulilojifunza kichwani kwako. Jaribu tena bila ya kuhofu labda utakosea tena. Kama tayari kuna somo umepata kwenye kushindwa kwako basi utakuwa na ujasiri wa kujaribu tena. Watu wengi hukata tamaa kabla hawajakaa chini na kujitazama ni […]

521; HEKIMA: Serikali Yako Ina Sheria na Taratibu?

Kila serikali huendeshwa kwa sheria na taratibu mbalimbali ambazo huwezesha watu kuishi kwa pamoja na kupunguza matatizo mbalimbali. Nimejiuliza kama mpaka sasa kungekuwa hakuna serikali, wala mipaka ya nchi yaani mtu peke yake anaibuka tu anafanya kila anachotaka tungekuwa wapi? Ukweli ni kwamba kuna vingi tungekosa na kuna vingi vingepotea. Sasa kama ni hivyo wewe […]