Mara nyingi unaweza kukutana na mtu anasema “Ningekuwa na Mtaji wa shilingi fulani ningefanya biashara Fulani” sasa ukimuuliza mawazo yako ni mazuri sana sasa unafikiri huo mtaji unaousema unatoka wapi? Kuna juhudi gani unafanya sasa hivi ili angalau uwe na huo mtaji? Mtu huyo ataanza kukupa maelezo ya kutosha kwanini haiwezekani na hali ilivyo mbaya.

Ukweli unabakia palepale hata hali ikiwa mbaya kiasi gani wewe kuendelea kutoa hiyo sababu ya hali ngumu, hali mbaya, haibadilishi chochote kwenye maisha yako. Kama umeona hali ni mbaya tafuta suluhisho tu.

Kutoa Sababu za Kwanini Upo Hapo Ulipo.

Kama wewe muda mwingi ukiulizwa kwanini upo hapo ulipo sasa na ni kitu gani kinakufanya ubakie hapo ulipo unaishia kuwa na sababu nyingi na za kutosha za kuelezea bila ya maelezo utafanyaje ili utoke hapo basi ujue utaendelea kubaki hapo. Pamoja na kwamba huwezi kukosa sababu za kuwepo hapo ulipo ndio lakini lazima basi uwe na angalau njia na namna ya kufanya ili utoke hapo ulipo.

Kuendelea Kufanya Kama Wanavyofanya Unaofanana Nao.

Kama utaendelea kufanya kama ambavyo wanafanya uliopo nao hatua zinazofanana basi ujue hakuna cha tofauti na wao utakachopata hata siku moja. Penda kuwatazama walipo mbele yako pia ili uweze kujifunza na kujua walitokaje kwenye hatua uliyofikia. Nenda hatua ya ziada tofauti na wenzako ili uonyoshe utofauti.

 

Kutokujifunza Chochote Kwa Waliokutangulia Kimafanikio.

Wewe hakuna unachojifunza kwa waliokutangulia unategemea nini? Waliokutangulia wamepitia katika njia ngumu sasa na wewe ukipita kwenye njia ngumu ni uzembe wako mwenyewe. Unapaswa ujifunze kwao ili kuepuka kurudia makossa ambayo wao walishayafanya. Kama kuna changamoto walipitia hutaweza kuirudia tena kwasababu utaweza kuona ni hatua gani walichukua kuivuka hiyo changamoto.

 

Kuacha Kabisa Kuhudhuria Mafunzo na Kusoma Vitabu.

Ukiulizwa mara ya mwisho umehudhuria semina lini hujui, vitabu umesoma mara ya mwisho lini hujui. Halafu unategemea usongeje mbele? Hujalisha ubongo wako unategemea matokeo gani ukupe? Unataka matokeo makubwa wakati hujajipa uwezo wa kuyapata hayo matokeo? Hivi unajua ng’ombe akiwa hajashiba vizuri na kupewa maji ya kutosha anataoa maziwa kidogo sana? Hivyo pia hata akili yako ikikosa chakula chake haiwezi kuwa na ufanisi katika kazi unazofanya.

 

Kupoteza Muda Mwingi Kwenye Mitandao ya Kijamii.

Muda wako unautumiaje? Unatumia muda mwingi kutazama habari na mambo ambayo sio msaada kwako kila wakati kuliko haya ambayo yangekutoa hapo ulipo halafu unataka usonge mbele? Badilisha unavyofanya kama unataka matokeo ya tofauti. Tumia muda wako vizuri ili ukuletee matokeo bora.

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

 

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua”

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading