Mara nyingi tumekuwa tukimtafuta mchawi wa mafanikio yetu hasa pale tunapokwama na kushindwa kwenda mbele. Tunasahau kwamba mchawi huyo tumembeba sisi wenyewe ndani yetu.
Wewe pekee ndio unatakiwa uweke bidii lakini umekuwa sababu ya kujirudisha nyuma kwa kuzembea yale ambayo ulitakiwa kufanya.
Wewe ndio una nguvu ya kuamua nani awe rafiki yako lakini mpaka sasa unaendelea nao sasa sijui unaogopa nini?
Wewe ndio umekuwa huweki akiba na madeni yamekuwa mengi sana na wakati mwingine unashindwa hata kufanya yale malengo uliyojiwekea.
Wewe pekee ndio unaamua kula vibaya na mwisho wako utaanza kupata magonjwa kama kisukari na presha mwisho wake ni afya mbovu na utashindwa kutimiza ndoto zako.
Wewe pekee yako ndio umeamua kutokuwa mwaminifu kwenye mahusiano yako na hata sasa yanakaribia kuwa mabovu au kuvunjika.
Chochote kibaya kinachoendelea kwenye maisha yako kwa namna moja ama nyingine wewe ndio unahusika kwa asiilimia nyingi Zaidi kuliko wengine katika kusababisha. Hivyo ni wakati wako kuchukua hatua sasa.
Hata kama utasema sio wewe lakini bado jukumu la kukutoa hapo ulipo lipo mkononi mwako. Hakuna mwingine atakae kuja akufanyie maamuzi. Na kama yupo basi wewe bado huna uhuru wako binafsi.
Hakikisha unajijengea nidhamu ya maisha yako ili uweze kuwa na maisha yeye manufaa. Kama maisha yako yanakuwa kero kwa wengine kama watoto wako, mwenzi wako basi kuna sehemu unakosea. Anza kujirekebisha uwe mtu ambae kila mmoja anatamani kuwa.
Wewe pekee ndio unatakiwa uanze kubadilika ndipo uweze kubadilisha marafiki. Huwezi kubadilisha marafiki wakati bado unatabia zile zile za siku zote. Watu wengine watakuogopa wakijua utawaambukiza tabia zako mbaya. Anza kubadilika kwanza ndipo ufikirie kubadilisha vitu vingine.
Ukiamua kuwa mwaminifu kwenye mahusiano inawezekana ni nidhamu tu inatakiwa. Ukiamua kuwa na tabia nzuri ya kufanya mazoezi inawezekana ni nidhamu tu inatakiwa.
Anza sasa wakati ni wako.
Your Partner in Success
Jacob Mushi
Success Motivator, Author & Entrepreneur

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading