Kamwe usitegemee kupata kinyume cha kile unachotoa. Kama utatoa chuki kwa watu utarudishiwa chuki. Ukionyesha upendo utapokea upendo.
Kutoa na kupokea ni sheria ya asili ambayo ndio inaongoza maisha yetu tangu zamani. Kwa matokeo yeyote unayopata kwenye maisha yako kabla hujalaumu au kutoa sababu mbalimbali jiulize wewe mwenyewe ulitoa nini?
Ukitaka kuonyeshwa upendo na wengi onyesha upendo. Ukitaka watu wakupe tabasamu wape tabasamu. Ukitaka kupata matokeo bora kwa wàteja wako wape kile wanachokihitaji.
Kama ukishindwa kuelewa kanuni hii utaishia kulalamika na kulaumu wengine, kulalamikia serikali, kusingizia hali ngumu na kadhalika.
Kiwango cha pesa ulizonazo sasa hivi ni kiwango cha thamani uliyotoa kwenye biashara yako au kwenye kazi ile uliyoajiriwa.
Kama unataka kuongeza kipato ongeza idadi ya unachotoa.
Kama watu wanashindwa kukuamini kuna vitu ulitoa wakashindwa kukuamini.
Tunalipwa kulingana na thamani tunayotoa. Ukitoa thamani kubwa utapokea malipo makubwa. Ukitoa vitu vya hovyo utapokea malipo ya hovyo.
Kama unataka kuongeza kiwango cha upendo, pesa au chochote kwenye maisha yako, anza kwa kuongeza thamani yako. Kuwa bora zaidi. Watu hawataangalia kiasi cha pesa wataangalia thamani ya kile unachowapa.
Karibu Sana.
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: 0654726668
E-mail: jacob@jacobmushi.com
Blog: www.jacobmushi.com
jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading