Watu wengi wanahamasika sana wakisikia neno mabadiliko lakini hawaelewi hasa ni vitu gani wanatakiwa kufanya ili wayapate. Tunapokuja kwenye kuchukua hatua ili kupata mabadiliko chanya wengi ndio huanza kukimbia na kurudia hali zao za kawaida.
Kuna watu wakisikia kuhusu mabadiliko huwa wanapenda sana na kufurahia lakini hawaelewi nini gharama gani wanatakiwa kulipa ili kupata mabadiliko wanayoyafurahia. Ili utoke kwenye hali uliyonayo sasa hivi unahitaji kulipa gharama.

Ukweli gharama ni kubwa sana na inahitaji kuvumilia ndio maana watu wengi hawabadiliki. Ndio maana watu wengi Maisha yao huwa yanarudi katika hali walizozizoea kama zamani.

Mabadiliko ni kipindi cha mpito ambacho wakati unakipitia unaweza kukosana na mwili wako uliokuwa umezoea starehe, kulala sana, kukaa bila kusoma na kadhalika.

Mabadiliko kutoka kwenye hali uliyonayo sasa kwenda kwenye hali nyingine yanaweza kukusababishia kukimbiwa na marafiki. Kukosana na watu unaowapenda maana utaanza kufanya vitu vya tofauti ambavyo hawajavizoea.

Unafikiri ni rahisi sana mtu kuacha kazi yake iliyokuwa inampatia mshahara wa uhakika kila mwezi halafu umwambie akapambane akautafute huo mshahara kwa kufanya biashara zake mwenyewe?
Unafikiri ni rahisi mtu tangu akiwa mtoto anaimbiwa soma kwa bidi uje upate kazi nzuri halafu leo amefika chou Kikuu anamaliza unaanza kumhamasisha tu aache kufikiria kuhusu ajira akajiajiri?


Sio kitu kirahisi ndio maana watu wanabaki na hali zao zile zile,
Sio kitu kirahisi ndio maana mtu ataanza biashara akikutana na ugumu Fulani anarudia Maisha aliyoyazoea.

Sio kitu cha siku moja lazima mtu aamue kabisa kutoka kwenye Maisha ambayo aliambiwa kwamba ndio ya kuishi.

Ukiamua kubaki kwenye hali uliyoizoea hatari yake ni kwamba utakuwa na hali mbaya Zaidi siku zinazokuja. Kama hutaamua kubadilika Maisha yako yatazidi kuwa magumu Zaidi.

Hivyo ni muhimu sana kutambua mabadiliko ni lazima hakuna namna ukiamua kubaki hapo ulipo utabadilika kwenda sehemu mbaya Zaidi. Mabadiliko rahisi sana ni kutoka sehemu nzuri uliyokuwa kwenda sehemu mbaya Zaidi mabadiliko haya yanaweza kutokea ndani ya siku moja tu. Mabadiliko mazuri na ya kuleta Maisha mapya kwenye Maisha yako hayatokei siku moja.
Your Partner in Success
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668/+255 755 192 418
jacobmushi.com.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading