Habari Rafiki, Leo ni siku nyingine tena ambayo tumepewa kama zawadi kwa ajili ya kwenda kuyafanya Maisha yetu yawe bora Zaidi.

Jisemeshe Maneno Haya Kabla Hujatoka Kwenda kufanya Chochote.

“NACHUKUA HATUA, NAJIFUNZA, NAWEKA JUHUDI NA BIDII, NAVUMILIA.
MAFANIKIO NI HAKI YANGU, EEH MUNGU NIWEZESHE.”

Kuna msemo usisubiri embe chini ya mnazi. Yaani kile unachokitaka siku zote kinapatikana kule kinapotakiwa kuwepo.

Ukikaa nyumbani halafu unasema maisha ya magumu ni wewe umeamua mwenyewe.

Ukikaa na wapumbavu halafu ukategemea uwe na maarifa utakuwa unajidanganya.

Penda kujihusisha na kule kunapoleta matokeo ya maisha yako.

Tunda siku zote halianguki mbali na mti wake, yale yanayowatoka watu ndio yamewajaa.

Kuna mtu anasema hali ni ngumu lakini muda wake mwingi kauweka kwenye kufuatilia maisha ya wengine.

Kuwa sehemu ambayo unatakiwa kuwepo lazima utaziona fursa.
Ukikaa sehemu za watu utaishia kulalamika siku zote.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi
#UsiishieNjiani
“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”
https://jacobmushi.com/patavitabu/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading