Maisha ni ya ajabu sana, unazaliwa bila idhini yako mwenyewe, pengine hata wazazi wako hawakutarajia wala kupanga wewe uzaliwe. Na hata kama wakipanga hawawezi kujua kabisa ni mtu wa aina gani anazaliwa, vipimo vinaweza kujua jinsia lakini haviwezi kujua ile jinsia imebeba mtu wa namna gani.

Kingine cha ajabu sana sasa ni kuwa hujui utakufa lini, huna uwezo wa kuamua ufe wakati gani, japo wapo wanaojaribu kujiua lakini bado wanakuwa hawapo sawa kiakili. Ni kitu cha ajabu sana kwasababu wapo wanaozaliwa na kufa papo hapo na wengine wanasogea umri hadi ujana na kisha kuondoka.

Kitu kimoja ambacho wewe unaweza kukitumia vizuri ni muda. Unaweza kufanya chochote kwenye muda wako wa kila siku. Unaweza kufanya chochote unachojisikia ukiwa bado hai. Wako watu wanaamua kufanya mambo ya ajabu yaani yale ambayo jamii imeyaita ni maovu. Wapo wengine wanafanya yale ambayo jamii inayaita ni mema. Kila mmoja anajitahidi kufanya kwa bidii sana kile alichochagua kufanya.

Wapo ambao wameamua kwenda mbali Zaidi na kufanya mambo makubwa kabisa na kuleta utofauti katikati ya wanadamu wenzao. Wote hao wametumia muda, wote hao hawakuchagua wazaliwe, na bado hawajui watakufa lini ila wana muda kama wa kwako.

Ukiamua kuutumia muda wako kuishi vile jamii inavyotaka uishi au vile ambavyo inasema ndio Maisha mazuri basi utakuwa kama jamii yako ilivyo. Ukiamua kwenda hatua za ziada basi unaweza kuwa mmoja wa watu wa pekee katika ulimwengu huu.

Nafasi ambayo kila mmoja anayo ni hii ya kutumia leo kufanya chochote kile anachokipenda. Niliandika kitabu cha SIRI 7 ZA KUWA HAI LEO kwasababu ya msukumo huu kwamba hakuna binadamu ajuae siku yake ya kuwa hai na wala hajachagua kuzaliwa. Hivyo basi ukifahamu haswa kile ambacho unataka na ukaitumia vizuri leo kufanya utaishia kwenye mafanikio.

Leo ndio inaleta mwezi, mwaka na miaka, kama utaweza kuitumia leo vizuri basi wewe Rafiki yangu hutakuwa wa kawaida. Kila mmoja anatumia leo yake kwa namna ya tofauti tofauti. Kuna waliokata tamaa na kuamua kuendelea kuishi Maisha ya kupigania uhai wao tu hapa duniani yaani kula kuvaa na kulala basi. Wapo walioamua kuja na mabadiliko na mwisho wa siku dunia nzima ikawa inatumia vile vitu ambavyo wao wamegundua.

Jitahidi Rafikiyangu na wewe angalau utoke kwenye ukawaida yaani uende hatua ya ziada ambayo wengiwanaogopa kufika. Ninaamini unaweza kile ambacho Mungu ameweka ndani yako badokina nafasi ya kufikia mwisho mkuu.

Ubarikiwe sana,

Rafiki Yako, Kocha Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/coach

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading