JALI CHANZO CHA MAFANIKIO YAKO.
Habari za leo ndugu msomaji wa mtandao huu wa Rise and Shine natumaini unaendelea vyema. Leo tunaenda kujifunza kuhusu kujali chanzo.
Chanzo cha hapo ulipofikia ni Mungu.
Elimu uliyonayo chnzo chake ni Mungu.
Jali chanzo cha mafanikio ya hapo ulipo.
Kumb.8:11-20
Tunakuwa na bidii sana wakati tunatafuta vitu tukisha vipata tunasahau kwamba Mungu ndie alietufikisha na kutulinda tukaweza kufika. Haijalishi umepata mafanikio kiasi gani ukisahau kua Mungu ndie aliekusaidia ni hatari sana kufilisika ni muda mchache.
Tunatakiwa  tujifunze sisi binadamu  kwa mfano. Mtu anapokua amekuja kwako ana shida ukamsaidia utajisikiaje atakapoondoka asiseme asante au shida yake inapoisha asipoonyesha shukrani kama binadamu hua hatujisikii vizuri. Je Mungu wetu wa mbinguni si zaidi?
Zaburi 136:1-26 
Umemuomba Mungu akakupatia jambo mshukuru kila siku Mshukuru nenda ibadani atakuzidishia zaidi na zaidi. Mshukuruni Bwana kwa kua ni mwema kwa maana fadhili zake ni za milele.
Tukija kwa upande wa binadamu vitu tulivyo navyo vinavyotuzalishia  mali lazima pia tuvijali. Kama unafuga ng’ombe anaekamuliwa maziwa ili atoe maziwa ya kutosha knabidi apewe chakula cha kutosha maji na pumba lasivyo maziwa hutopata.
Kitu chochote kinachokuletea mafanikio lazima ukijali ili mafanikio yako yazidi kuongezeka. Ukifurahia mafanikio ukasahau chanzo ujue umeanza kupotea.
Asante sana kwa kusoma makala hii. 
Imeandikwa na Jacob Mushi

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading