Mtu anatengenezwa katika umri wa kuzaliwa mpaka anapokuwa na miaka 7. Tabia Nyingi na Imani ambazo unazo sasa zilijengwa ulipokuwa mtoto. Na mara Nyingi Imani hizi zilijengwa ulipokuwa unaona kile ambacho watu wa karibu na wewe wanafanya.

Mtoto anapozaliwa ubongo wake wa kumbukumbu unakuwa mtupu kabisa. Hivyo kila ambacho anaona kinafanyika kinaingizwa kwenye ubongo wa kumbukumbu na anaona hayo ndio Maisha anayotakiwa na yeye aje kuishi. Ni mkuhimu sana kuwa makini na kile ambacho unamfanya mtoto wako aone kipindi hiki kwasababu ndio wakati unatengeneza mfumo wa Maisha yake.

Umaskini unatengenezwa wakati huu wa utoto, tabia mbalimbali mbaya na nzuri zinajengwa kipindi hiki cha utoto. Kuna nafasi kubwa sana yam toto kuja kuwa mlevi kama baba yake alikuwa mlevi alipokuwa mtoto. Pia kuna nafasi kubwa ya mtoto kuchukia pombe kwasababu hiyo hiyo ya kuona baba yake alipokuwa mlevi.

Mfano, kuna Watoto wawili mmoja anamuona baba yake anakuwa mlevi sana na kila siku wanakwenda kumuokota mtaroni. Mmoja anaweza kujenga mtazamo kuwa haya ni Maisha mabaya sana kama amewahi kuona watu wengine wenye Maisha bora Zaidi na Maisha yake yote akawa anauchukia ulevi. Mtoto mwingine anaweza kuona haya ndio Maisha na akajijengea tabia ya ulevi anapokuwa mtu mzima.

Mtoto anaweza kuuchukia ulevi kwasababu aliona baba yake akija akiwa amelewa hua anampiga mama kila siku na wakati akija akiwa hajalewa analeta Zawadi na nyumbani kunakuwa na Furaha. Chochote kila ambacho mtoto anakiona anatengeneza Imani ndani yake. Na Imani hizi ndio zinayajenga Maisha yake ya Baadae.

Kuna tabia Nyingi ambazo zinawatesa watu zilizjengwa ukiwa katika umri huu wa mtoto. Hali ya Maisha unayoteseka kuibadilisha sasa hivi imeletwa na Imani ambazo ulizijenga au kujengewa ulipokuwa mtoto.

Ukitaka kujua huu ni ukweli angalia pale unapotaka kufanya jambo lolote ambalo hujawahi kufanya kunakuwa na sauti mbalimbali zinakuja ndani yako. Nyingine zinakwambia huwezi kwasababu hujawahi kufanya, nyingine zinasema ulishwahi kushindwa hapa na pale na kukufanya ujawe na hofu ndani yako.

Rudia Rudia Rudia.

Ipo njia ya kutengeneza Imani mpya na kuondoa kabisa zile Imani ambazo ulizijenga ukiwa mtoto mdogo. Njia hii ni kurudia rudia tabia ambayo unataka kuijenga. Tunaweza kusema unatakiwa ufanye kila siku kile ambacho unataka kukijenga upya ndani yako.

Unatakiwa urudie mpaka pale ile Imani mbaya ambayo umejengewa ndani yako iondoke kabisa. Hii sio zoezi la siku moja, wapo wengi wamejaribu ndani ya siku kadhaa wakaishia njiani. Lakini unatakiwa utambue kwamba haya mambo umejengewa kwa Zaidi ya miaka 7 huwezi kuja kuyaondoa kwa siku chache tu. Lazima ukubali kujitoa vya kutosha kurudia rudia hadi uweze kufanya zile tabia ambazo umekuwa unataka kuzitengeneza kwenye Maisha yako.

Leo chukua kitabu chako ambacho unaandika mambo yako ya muhimu andika yale mambo ambayo huyataki kwenye Maisha yako. Andika zile tabia mbaya na utafute tabia nyingine nzuri za kubadilisha na hizo tabia mbaya unaze kuzifanyia kazi.

Tengeneza Picha Mbaya.

Kama unavuta sigara basi tengeneza picha mbaya ukiwa unaugua saratani kwasababu unavuta sigara. Kama unajichua embu tengeneza picha mbaya kwamba baada ya miaka michache utakuwa na mgogoro kwenye mahusiano yako.

Kama unalala sana embu tengeneza picha ukiwa ni maskini sana kwasababu unapenda sana usingizi. Halafu jiulize unataka kuyapata hayo matokeo? Kwasababu ni matokeo mabaya basi yatakuwa unayakumbuka kila unapotaka kufanya hizo tabia mbaya.

Tafuta Mtu Unaemwamini.

Tafuta mtu ambaye unamwamini na kumheshimu mwambie unataka kuacha tabia Fulani na Fulani na utakuwa unafanya vitu kadhaa kila siku. Kazi yake huyo mtu ni kukufuatilia wewe kujua unaendeleaje na umefikia wapi. Unaweza kumwambia awe anakufuatilia kila siku endapo hizo tabia umekuwa unazifanya kila siku.

Tafuta Kocha.

Unaweza kutafuta Kocha ukamlipa na akakuongoza katika kutengeneza tabia mpya ambazo unataka kwenye Maisha yako. Ndani ya muda Fulani unakuwa tayari umeweza kutengeneza kile ambacho unakitaka.

Ni kweli ni ngumu sana kuacha inawezekana unajisemea sasa nimejaribu sana lakini nimeshindwa, nataka nikwambie ni ngumu ndio lakini ugumu mbaya Zaidi ni wewe kuendelea kubaki na tabia ambazo unazo sasa hivi.

Nikutie moyo kwamba inawezekana kubadili chochote unachokitaka kwenye Maisha yako. Inawezekana kutengeneza mfumo wa Maisha ambayo unaufurahia kila siku. Ukiamua kuchukua hatua kila siku inawezakana kubadili Maisha yako.

Kama unatafuta Kocha Unaweza kunipa mimi hiyo nafasi nikawa Kocha wako. Bonyeza Hapa…. https://jacobmushi.com/kocha/

Ubarikiwe sana,

Rafiki Yako, Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/huduma

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading