Maisha yako ni vile vitu ambavyo unavifanya kila siku ana kwa kuvifanya kila siku vinakwenda kuwa tabia yako. Muunganiko wa tabia zako unatengeneza kitu kinaitwa mfumo wa maisha. Huu mfumo wa maisha ni muunganiko wa tabia ndogo ndogo ambazo unazifanya kila siku.

Kama tabia zako ni mbaya basi mfumo wako wa maisha utakuwa mbaya.

Kama tabia zako ni za kimaskini maisha yako yatakuwa ya kimaskini.

Kama tabia zako ni za kivivu maisha maisha yako yatakuwa magumu sana.

Ukitaka kubadili chochote kwenye maisha yako angalia ni tabia gani hasa unapaswa kuzitengeneza uwe unaziishi kila siku.

Bahati nzuri tabia ulizonazo sasa hivi nyingi sio za asili nyingi umezitengeneza hapa duniani mwenyewe. Nyingine zimetokana na jamii uliyokulia. Nyingine umejifunza kutoka kwa marafiki na nyingine kwenye mifumo ya taarifa kama kwenye tv na movies.

Unaweza kuandika leo tabia ambazo unazitaka ili uweze kufikia mafanikio. Kutokana na maono uliyonayo unatakiwa ujue ni aina gani ya tabia nikiitengeneza na kuifanyia kazi kila siku itanipekeleka mimi kwenye ndoto zangu.

Soma: JINSI YA KUSHINDA CHANGAMOTO

Haiwezekani unachukia kitambi halafu ukaishi maisha ya kula vyakula ambavyo unajua fika kabisa vitakuletea kitambi. Lazima utachagua vyakula visivyoleta kitambi. Hivyo hivyo kwenye mambo mengie utaka taka kuwa na pesa nyingi tengeneza tabia, weka akiba , jifunze uwekezaji, fanya biashara usitegemee chanzo kimoja cha kipato.

Hivyo kwenye mahusiano na pia kwenye roho yako. Kila unachokitaka unaweza kukipata kwa kutengeneza tabia ambazo utaziishia kila siku na zikuletee matokeo ya kile anachokitaka.

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

 

Jacob Mushi,

Author, Entrepreneur, Trainer, Life Coach,

Simu: 0654 726 668,

Twitter: jacobmushitz

Instagram: jacobmushi

Facebook: Jacob Mushi Page  

Barua pepe: jacob@jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading