Habari Rafiki yangu. Utakuwa umeshtuka sana kusoma kichwa cha Makala hii, ukweli ni kwamba mwaka 2018 ndio umeisha hivyo. Tunasema imeabaki miezi miwili kwasababu mwezi wa 12 hatujauweka kwenye ratiba watu wengi ndio huenda likizo za kazi, wengi ndio mwezi wa kusherehekea. Itaendelea kubaki miezi mitatu kwa wale ambao wana biashara zao binafsi na lazima wafungue ili wawahudumie wale ambao wamerudi likizo.

Usishangae sana yale ambayo ulisema utafanya mwaka huu sasa hivi bado hujafika hata robo yake. Kitu cha ajabu ni kwamba bado unataka tena kuahirisha na kusema utaendelea tena mwakani. Usikubali kukata tamaa mapema hivyo hii miezi iliyobaki bado unaweza kufanya kitu kikubwa na ukatimiza malengo yako kwa asilimia kubwa sana.

Vitu vya Kufanya;

Fanya Tathimini ya Malengo Yako Mwaka Huu.

Ndio rudi tena kwenye kile kitabu chako ulipoandikaga malengo yako yam waka uanze kuyapitia upya moja baada ya jingine. Angalia ni vingapi umeshafanya na mangapi umegusagusa tu, na ni yapi hata hukuyakumbuka tena.

Nataka nikwambie hakuna wa kumlaumu, sio Magufuli kabana, hali ngumu kipindi hiki, mambo yalikuwa hovyo au sababu yeyote ile ambayo unataka kutoa. Hizo sababu hazibadili kitu. Wewe ndie unawajibika kwa Maisha yako. Usipotimiza malengo yako ni wewe mwenyewe unapata aibu na fedheha.

Andika yale yote ambayo hukuyatimiza uanze kuyafanyia kazi upya miezi hii mitatu iliyobaki. Chagua malengo machache makubwa ambayo unataka angalau kwenye miezi hii mitatu uweze kuyatimiza.

Yagawanye Malengo Yako Katika Mpango Kazi wa Wiki.

Yale malengo uliyochagua yagawanye kwa mpango wa wiki kama ulisema utaandika kitabu na hukuandika. Weka lengo la kuandika kurasa kadhaa kwa wiki. Mfano; unataka kuandika kitabu chenye kurasa 300 sasa weka mpango wa kuandika kitabu hicho ndani ya mwezi huu wa kumi, ambapo utagawanya kwa 4 utapata kurasa 75 kila wiki. Maana yake wewe kila wiki unatakiwa uandike kurasa 75 za kitabu chako. Ukigawanya kwa siku maana yake kila siku angalau uweze kuandika kurasa 10.

Unaweza kugawanya malengo yako kwa mfumo wowote ule unaoutaka ili mradi uweze kuufanyia kazi vizuri na upate yale matokeo unayotaka. Bila kugawanya malengo yako utayaona ni makubwa sana na utaishia njiani. Anza Kuchukua Hatua Sasa yaani kuanzia kesho tarehe moja.

Tafuta Kocha/Mtu Unaemheshimu akusimamie na Kukuongoza.

Ni kweli itakuwa ngumu sana kutimiza mwenyewe kile ambacho ulisema utafanya mwaka huu na umekiahirisha mpaka sasa. Inakubidi ukubali kuwa Mwanafunzi wa mtu, kuna yule mtu ambaye unamheshimu sana ukimwahidi kitu basi unajitahidi kwa namna yeyote ile ukitimize. Mtafute huyo mtu leo umpigie mueleze malengo yako mwombe akusimamie mpaka yatimie.

Tafuta kocha ambaye atakuongoza, mlipe gharama kabisa ili uweze kujitoa kisawasawa kwenye lile lengo lako. Usikubali kuchukulia kirahisi mafanikio yako. Kama kweli lengo lako lina thamani hutaona gharama kubwa sana kutafuta mtu wa kukuongoza na umlipe kiasi kidogo cha pesa akusimamie miezi hii iliobaki hadi utimize malengo yako.

Usikubali kabisa mwaka huu upite tena kama miaka mingi ambayo ulikuwa unasema utafanya, utafanya kesho. Usikubali kuendelea kuahirisha malengo yako kila wakati. Hayo ni Maisha yako usipoyapa kipaumbele basi ujue hakuna ataekuja kuyapa kipaumbele.

Nataka nikwambie wewe mwenyewe ndie una Ndoto zako na malengo yako na Ndoto zako. Wewe ndie mwenye majukumu ya Maisha yako. Usipoyachukulia hatua hakuna kitakachokwenda kutokea.

Ukihitaji niwe kocha wako nikuongoze utimize malengo yako bonyeza hapa www.jacobmushi.com/kocha

 

Ubarikiwe sana,

Rafiki Yako, Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/huduma

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading