527; HEKIMA: Kinyozi Anapokosea Kukunyoa.

Kinyozi anapokosea kukunyoa bila kujali amekosea kiasi gani siku zote baada ya muda Fulani nywele huota tena na utaweza kunyoa vile unavyotaka. Unapopoteza fedha haijalishi ni nyingi kiasi gani kama ni wewe mwenyewe ulizitafuta basi utaweza kuzipata tena. Unapoachwa na mpenzi ambaye ulimpenda sana bila kujali alikuwa mzuri kiasi gani, bado ipo siku utakuja kukutana […]

526; HEKIMA: Sumu Niliyowekewa Kwenye Chakula.

“Ilikuwa ni siku za mwisho wa mwaka ambapo tulikuwa na utaratibu wa kwenda kuwasalimia ndugu na jamaa ambao hatujawaona miaka mingi. Katika kuwatembelea ndugu jamaa na marafiki wengi siku moja nikapitia kwa ndugu mmoja ambaye hatukuonana muda mrefu sana. Huyu ndugu baada ya kunipokea alinisisitiza sana nile chakula. Nilimkatalia kwasababu nimepita nyumba nyingi na nimeshakula. […]

525; HEKIMA: Ni Wewe.

Ni wewe utawajibika pale unapoingia kwenye matatizo bila kujali ni nani aliyeyasababisha. Ni wewe utatakiwa kuchukua hatua pale mambo yanapokuwa magumu kwasababu ya uzembe unaoufanya sasa. Ni wewe utakalipa gharama za ulaji mbovu unaokula sasa pale utakapoanza kusumbuliwa na magonjwa. Ni wewe utakaelipa gharama ya ujinga unaoundekeza sasa hivi, unaambiwa ujifunze hutaki, Unaambiwa uweke akiba […]

514; HEKIMA YA LEO Upendo Ni Amri

Siku zote amri inapotolewa kinachofuata huwa ni Utii na unaposhindwa kutii amri maana yake wewe unakuwa muasi. Kwa serikali zetu ukiasi kinachokujia ni hukumu wakati mwingine hata kifo kutegemea na yule aliekupa amri. Sasa tukisoma kwenye neno la Mungu Yohana. 13:34 Amri mpya nawapa, Mpendane. Maana yake kupendana na ndugu zako, watu waliokuzunguka, ni amri sio […]

509; Penda Tatizo Unalotatua.

Nipo natazama nyimbo YouTube nimekutana na wimbo uliwekwa mwaka 2009. Huo wimbo kwa mimi kuutazama leo pamoja na wengine wengi huyo mwimbaji atalipwa na YouTube (Google) mamilioni ya pesa. Nilichojiuliza ni kwamba huyu mwimbaji wakati anatunga wimbo huenda hakuwahi kuwaza kama mwaka huu 2019 huo wimbo wake bado ungeendelea kuingizia pesa. Nataka niseme na wewe […]

KITABU: NUKUU ZA MAISHA.

Nukuu za Maisha (Malengo, Mafanikio, Mahusiano n.k) ni Kitabu kinachokupa muongozo wa maneno ya kutafakari kila siku asubuhi ili uweze kuwa na siku bora na yenye mafanikio. Kitabu hiki kina nukuu 400+ ambazo zinakupa uwezo wa kufikiri vizuri, kuishi kwa furaha na kuweza kusonga mbele katika kile unachokifanya. Nukuu za Maisha ni mjumuisho wa nukuu […]