Kulikuwa na Bwana Mmoja alikuwa anafanya biashara ambayo inamlazimu sana kuzungumza na watu kila wakati. Yaani ili auze lazima aongee na mtu.

Sasa kwasababu hiyo akajikuta anashauriwa sana na watu wengi. Kila mtu anaekutana nae anajaribu kumwelekeza njia nzuri ya kuifanya biashara yake.

Siku moja akatafuta mtu mwenye hekima ili amshauri juu ya ushauri anaopokea kila siku.

Akakutana na mzee mmoja mwenye hekima sana. Mzee yule baada ya kumsikiliza akamjibu kwa kifupi sana.

Akamwambia “Kijana wangu ukitaka kufanikiwa kwenye hiyo biashara yako, Usipokee ushauri wa aina yoyote na wala usitoe ushauri wa aina yoyote wa bure.”

Kijana wa watu akabaki anashangaa tu. Ila akaja kuelewa siku moja mzee alikuwa anamaanisha nini.

Ukitafakari sana kwenye Maisha yetu kuna watu wengi wanaweza kutushauri juu ya vile tunavyofanya.

Wengi wanatushauri kwa kututakia mema kabisa lakini kwasababu hawajui wanachokishauri vizuri wanaweza kutupoteza.

Ushauri ambao hulipii gharama yoyote mara nyingi gharama zake zinaweza kuja kuwa ni hasara au maumivu utakayopata baada ya ushauri kufeli.

Unapoambiwa usipokee wala Kutoa Ushauri wa bure maana yake ukipokea ushauri wa bure utaumia na ukitoa ushauri wa bure utakuja kulaumiwa.

Unaweza kumshauri mtu aachane na mtu anaempenda kwasababu tu alikuwa anamtesa halafu kesho ukashangaa wanaendelea pamoja.

Amua sasa kubadilika lipa gharama ili uweze kwenda viwango vikubwa zaidi.

Nakutakia kila la Kheri

Rafiki Yako

Jacob Mushi

2 Responses

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading